STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 29, 2013

Msiba! Askofu Mosses Kulola katutoka duniani

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God hapa nchini Dk.Moses Kulola (pichani), amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa za kifo cha askofu huyu maarufu zimetolewa na mtoto wake Mwiinjilisti Daniel Kulola ambaye ameitoa kupitia mtandao wa face book ambapo ameueleza umma wa watanzania kuwa baba yake mzazi amefariki dunia katika hospitari ya Aga Khan ambako alikuwa amelazwa.
Hajaeleza marehemu alikua anaumwa nini lakini taarifa zinasema amekuwa mgonjwa siku nyingi ambapo aliwahi kulazwa nje ya nchi na baadae akarudishwa nchini na hatimae kufariki Dunia.
Hadi hivi sasa haijajulikana askofu kulola atazikwa lini lakini pia taarifa zimethibitishwa rasmi kutoka kwa wachungaji mbalimbali ambao wako chini ya kanisa lake ambalo lina mtandao nchi nzima na lenye waumini zaidi ya milioni 5 nchini kote.
 Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule  ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Alimwoa Elizabeth na wamezaa  watoto 10 ambapo saba bado hai.
Alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa. Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. 
Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.
Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.
Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuan makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo.
Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila. Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake. 
Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana, katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola na injili iliyonyooka na akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele bure.MUNGU ambariki sana mtumishi wake huyu ni mfano hai kwa watumishi wa MUNGU wa sasa.
BWANA Ametoa na BWANA pia Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment