Na Suleiman Msuya
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ipo
katika mkakati wa kuhakikisha kuwa huduma zake zinapatikana kwa njia ya mtandao
kieletroniki (online registration) ambapo kwa kuanzia imekwisha weka baadhi ya
nyaraka za mafaili kwenye mfumo huo.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja Huduma, Utawala
na Fedha Bosco Gadi wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii leo jijini
Dar es Salaam.
Alisema pamoja na kujipanga kuingia katika mkakati
huo wa kieletroniki pia wapo mbioni kurahisisha njia za malipo kwa kutumia
mabenki ambapo kwa sasa wamekubaliana na CRDB na NMB na mpango huo utaanza
Julai 15 mwaka huu katika benki ya CRDB.
Gadi alisema mpango huo utasaidia wadau kulipa ada
za usajili kwa njia ya benki popote walipo, pia mfumo huo utasaidia
kuwahakikisha kuwa wadau kupata huduma zote ambazo zinasimamiwa na BRELA.
“Tupo kwenye mchakato wa kutoa huduma katika njia ya
kieletroniki pamoja na wadau kulipia kupitia benki ambapo kwa sasa tumeanza na
CRDB kuanzia Julai 15 mwaka huu,” alisema.
Aidha Kaimu Meneja huyo wa Huduma, Utawala na Fedha
alisema BRELA katika kuhakikisha kuwa dhana ya ushirikiano na Sekta Binafsi
yaani PPP inafanikiwa imeingia mkatapa wa ushirikiano na Chama Cha Wafanyabiashara
na wenye Viwanga na Kilimo Tanzania (TCCIA) ili waweze kutoa huduma saidizi za awali za kusajili
makampuni na leseni za biashara katika ngazi ya Mikoa na Wilaya Tanzania Bara.
Gadi alisema kuchaguliwa na TCCIA kunatona na
taasisi hiyo kuwa na mtandao mpana wa kieletroniki unaounganisha ofisi zao za
Wilaya takribani nchi nzima kwa upande wa Bara.
Alisema wateja wa BRELA waliopo Wilayani na Mikoani
wanaombwa kutumia ofisi za TCCIA kwani maombi yao yatawafikia makao makuu bila
tataizo lolote.
Kaimu Meneja alisema mfumo huo ambao ulianza Desemba
mwaka 2012 umeonyesha mafanikio makubwa
ambapo hadi sasa maombi 500 yamefanikiwa kusajiliwa kupitia TCCIA.
Aidha alisema kupitia utaratibu huo unagharimu
shilingi 6,000 za uasajili wa jina la biashara ambazo zinalipwa BRELA na
shilingi 2,000 ambazo zinalipwa kwa ajili ya masuala ya utawala na kutumwa kwa
maombi.
Pia aliweka bayana kuwa kwa upande wa makampuni ada
ya usajili inayotakiwa kulipwa itategemea na kiasi cha mtaji cha mteja
anachokiandika kwenye katiba ya kampuni anayotarajia kuisajili.
Kwa upande wake Naibu Msajili wa BRELA Andrew Mkapa
alisema ofisi yao haitosita kuichukulia kampuni au biashara ambayo inaenda
kinyume na sheria zinazoiongoza BRELA.
Alisema ni vyema watu na kampuni ambazo zinasajiliwa
kufuata taratibu ziliopo katika katiba zao pamoja na zile za BRELA.
Mkapa alisema iwapo kampuni au leseni ya biashara
itaonekana kuvunja sheria kuna taratibu za kumtaarifu muhusi ambapo itakuwa ni
ya muda wa miezi mitata na iwapo hakutakuwa na majibu sahihi uamuzi wa kuifuta
utafanyika.
No comments:
Post a Comment