Waziri Kabaka |
Na Suleiman Msuya
WAKATI mchakato wa kuundwa katiba mpya ukiwa
umefikia hatua ya kupata maoni ya juu ya rasimu ya katiba Baraza la Vijana la
Taifa (JUVITA) limeibuka na kumtaka Waziri wa Ajira na Vijana Gaudensia Kabaka
na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba kuhakikisha Baraza
hilo linatajwa kwenye katiba.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiyi wa JUVITA Fahami
Mastawilly wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema dhumuni la JUVITA ni kuhakikisha kuwa vijana
wa Kitanzania wa kada zote bila kuangalia elimu zao wanakuwa na chombo ambocho
kitakuwa kinawawakilisha katika vyombo vya maamuzi.
Mastawilly alisema wanaamini kupata nafasi ya
kuonana na viongozi hao wawili kunaweza kusaidia ombi lao kufanyiwa kazi ili
kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa ni sehemu muhimu katika nchi na kuondokana na
hali ilivyo sasa.
“Jamani ndugu zangu wanahabari kwa muda mrefu
tumekuwa tukiomba baraza la vijana kutambulika rasmi katika katiba lakini
tunaona kuwa hatusikilizwi hali ambayo hatuwezi kuivumilia tena kwani tunaamini
ni haki yetu,” alisema.
Alisema wao kama vijana waanzishili wa harakati hizo
wameshindwa ni kwa nini Tanzania haitaki kuweka baraza la vijana ndani ya
katiba wakati ipo mifano ya nchi nyingine ambazo mabaraza yapo kama Kenya,
Uganda, Urusi, Ujerumani, Uswisi, Costarica na zingine nyingi.
Mwenyekiti huyo wa JUVITA alisema ni vema maoni
yatakayotolewa kupitia mabaraza ya Wilaya kwenye rasimu vijana wote bila
kuangalia itikadi zao za kisiasa, kidini, kabila na welimu wanatakiwa kuungana
na kuwataka wajumbe wa mabaraza kusisitiza kuwa ibara ya 43 ya rasimu kutaja
wazi uwepo wa baraza la vijana katika katiba.
Alisema ibara hiyo inatamka kuwa kila kijana ana
haki ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania pamoja na jamii kwa ujumla na kwa mantiki hiyo serikali
itawawekea mazingira, hali ambayo vijana wanahitaji kuwa pasomeke kuwa serikali
itahakikisha kuwa vijana wanawekewa chombo cha kuwaunganisha na kuwawakilisha
katika vyombo vya maamuzi nchini bila kujali itikadi zao.
No comments:
Post a Comment