STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 10, 2013

Waliochaguliwa kujiunga Kidato cha 5 na Vyuo hawa hapa!

Picture: Mulugo akitangaza majina ya Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi 2013
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akitoa taarifa leo juu ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa shule ya serikali na vyuo vya ufundi, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utawala Rasilimali Watu

Maelekezo kwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano, vyuo ufundi na chuo cha 'manegement' na maendeleo ya maji

  • Wanafunzi Kuripoti katika shule walizopangwa.Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kuanzia mwaka huu 2013 itaanza mwezi Julai. Wanafunzi wamepangwa katika shule zenye miundombinu na walimu kwa masomo husika. Aidha, kama baadae upungufu utajitokeza, wakuu wa shule wameelekezwa kufanya taratibu za kuazima walimu wa muda na kutoa taarifa kwa uongozi wa halmashauri husika kuhusu upungufu wa walimu uliopo.


Kwa nafasi hii, ninaagiza wanafunzi wote kuripoti katika shule walizopangwa tarehe 29 Julai, 2013. Kama kutakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kuhamia shule nyingine, uhamisho wa kawaida utafanywa baada ya kuripoti shuleni kupitia kwa mkuu wa shule husika, Mkurugenzi wa Halmashuri/Manispaa na Katibu Tawala wa Mkoa. (Wizara haitabadilisha shule walizopangwa wanafunzi)

  • Wanaporipoti wanatakiwa kuwa na:Original Result slip na Living Cerificate


No comments:

Post a Comment