STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 10, 2013

Uganda The Cranes kutua kesho kuivaa Stars

Uganda The Cranes katika picha ya pamoja
Na Boniface Wambura
KIKOSI cha timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Julai 11 mwaka huu) tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

The Cranes itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda ambapo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo.

Waamuzi wa mechi hiyo ambao wanatoka Burundi nao watawasili kesho saa 9.35 kwa ndege ya Kenya Airways. Naye Kamishna wa mechi hiyo Tesfaye Gebreyesus kutoka Eritrea atatua nchini keshokutwa alfajiri kwa ndege ya EgyptAir.

Maofisa wote hao wa mechi hiyo watafikia hoteli ya New Africa. Mkutano wa maandalizi ya mechi utafanyika Ijumaa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa, na utakuwa chini ya Gebreyesus.

Kikosi hicho jioni ya leo kilitarajiwa kushuka dimbani kuvaana na timu ya vijana ya U20 ya nchi hiyo baada ya kushindwa kuzipata timu za Sudan na Rwanda kwa mechi za kirafiki za kujiandaa na pambano hilo dhidi ya Stars..

No comments:

Post a Comment