Mchungaji Mtikila |
Na Suleiman Msuya
MWENYEKITI wa Chama Cha Democratic Party (DP)
Mchunga Christopher Mtikila amesema wapo katika hatua za mwisho za kisheria za
kufuta mchakato mzima wa kuandaa katiba kwani ni kinyume cha sheria.
Mtikila alibainisha nia yake hiyo leo jijini Dar es
Salaam wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii.
Alisema jamii inaweza kumshaanga hasa kwa ile ambayo
haijui kinachofanyika katika mchakato huo ila anaamini kwataweza kutambua
baadae nini anachakifanya kwa maslahi ya Watanzania hasa wale wa Bara ambao
yeye anawatambua kama Watanganyika.
Mwenyekiti huyo wa DP alisema iwapo Serikali
inahitaji kuwepo kwa katiba mpya ni vema muungano ukavunjwa kwanza kwani
muungano unaotajwa kuwepo haupo kisheria jambo ambalo limegharimu Taifa
kupoteza fedha nyingi bila kujulikana sababu za msingi.
“Ni jambo ambalo litawashangaza watu lakini nataka
mtambue kuwa mimi nafanya vitu kwa umakini sana na ndio maanda kesi nyingi
ninazofungua nashinda kutokana na ukweli kuwa najua nini nafanya kwa maslahi ya
Watanzania naamini kwa hili pia nashinda,” alisema.
Alisema suala la katiba limechukuliwa kisiasa zaidi
bila kuangalia uhalali wake hivyo hayuko tayari kuona jamii ikitengenezewa
katiba yenye misingi ya watu wachache ambao wanahija kujijengea maslahi yao.
Mtikila alisema mchakato wa katiba alianzisha yeye
mwaka 1986 hadi 1988 lakini alipata upinzania kwa kile anachodai kuwa ni
upinzania kutoka kwa viongozi ambao walijua kuwa anachokifanya ni haki ya watu
wengi.
Alisema ni vema jamii itakatambua kuwa suala la
katiba sio la mtu kuunda tume anayoitaka kufanikisha zoezi hilo kwani ni
dhahiri kuwa upo uwezekano wa kupata katiba ambayo itakuwa imeegemea katika
maslahi yake.
No comments:
Post a Comment