STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 10, 2013

Yanga kujiuliza kwa Rhino Rangers siyo Mtibwa tena

Chuji na Mbuyi Twite wakiwajibika uwanjani
BAADA ya kuchezea kichapo toka kwa Express ya Uganda, Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga kesho  Alhamis watashuka katika dimba la Ally Hassain Mwinyi mjini Tabora kupepetana na Rhino Rangers badala ya  Mtibwa Sugar ya Morogoro kama ilivyokuwa imetangazwa.

Huo utakuwa mchezo wa tatu kwa Yanga ambayo ipo katika ziara ya kimichezo Kanda ya Ziwa baada ya Jumamosi  kutoka suluhu ya bao 1-1 na Express ya Uganda jijini Mwanza, kabla ya  kufungwa 2-1 na Express katika mechi ya marudiano iliyochezwa jana mjini Shinyanga.
Hata hivyo ilielezwa kuwa Yanga ingecheza na Mtibwa Sugar, lakini mipango ya Mtibwa kutua mjini humo imeshindikana na hivyo kupewa nafasi hiyo Rhino Rangers ambao awali ilielezwa isingeweza kucheza mechi hiyio.
Mabingwa hao wanaitumia michezo hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Nationwide ni maalum kwa ajili ya kupeleka taji lao kwa mashabiki wao wa Kanda ya Ziwa na pia kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu msimu mpya itakayoanza Agosti 24.

No comments:

Post a Comment