STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 11, 2013

Barcelona yavuna hasara kwa David Villa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXVdAubyzc3VRBhsgwQL9vXIemtlKYc-fmp2oUoG_BoZRESn5CyLHIqG8HjzbRGHLD9CsZakcJ6ZKYKAsha-cecocQS34dyriNCsIBpq6d30gtujkaoH_mROv1j1j7wHVuodPX91g29qns/s320/David+Villa-9.jpg
David Villa

BARCELONA, Hispania
KUUZWA kwa mshambuliaji David Villa kwa klabu ya Atletico Madrid kumefichua siri ya hasara kubwa ya kibiashara kwa Barcelona kwenye soko la uhamisho katika miaka ya hivi karibuni.
Villa ameenda kuichezea Atletico kwa ada ya uhamisho ya euro milioni 5.1, tofauti na alivyosajiliwa kutoka Valencia miaka mitatu iliyopita kwa kitita cha euro milioni 40.

Imeelezwa kuwa Barcelona wamepoteza zaidi ya euro milioni 170 katika usajili wa wachezaji nane tu wa hivi karibuni, licha ya kwamba uhamisho wa Villa si uliotia hasara kubwa zaidi.
Orodha ya usajili ulioleta hasara kubwa (kwenye mabano bei ya hasara, bei ya kununulia kutoa ya kuuzia):
1. Zlatan Ibrahimovic (euro milioni -63)
2. David Villa (euro milioni -34.9)
3. Henrique (euro milioni -16.5)
4. Hleb (euro milioni -15)
5. Keirrison (euro milioni -14)
6. Caceres (euro milioni -13)
7. Chigrinsky (euro milioni -10)
8. Maxi Lopez (euro milioni -4)
Jumla: Euro milioni 170.4 hasara.

No comments:

Post a Comment