Hapo
ni abiria wa Basi hilo la Taqwa wakisubiria Masaada ili waendelee na safari yao.
|
Muonekano wa Basi la Kampuni
ya Taqwa baada ya kupata ajali na Watu 11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar
es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina
ya Center wilayani Mbarali.
|
WATU 11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la
kampuni ya Taqwa walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda
Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center
wilayani Mbarali.
Ajali hiyo
mbaya ilitokea juzi majira ya saa 2:00 usiku katika mtelemko wa mlima Mambi
katika barabara Kuu ya Mbeya –Iringa wilayani Mbarali ikihusisha basi la Kampni
ya Taqwa lenye namba za usajili T 396 AXZ na lori aina ya Center lenye namba za
usajili T 175 BRA.
Baadhi ya
watu walikuwa ndani ya basi hilo walisema kuwa wakati basi hilo likiwa kwenye
mwendo mkali katika mteremko huo, lori aina ya Center ambalo lilikuwa
likipandisha lilijaribu kupita gari lingine lilikuwa limesimama kando ya
barabara, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso na kusababisha basi hilo
kupoteza mwelekeo na kupinduka mtaroni.
Getruda
Kambale ambaye ni raia wa Congo, ni miongoni mwa abiria walionusurika kwenye
ajali hiyo ambaye alisema kuwa licha ya basi lao kubondeka vibaya, hakuna mtu
aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya abiria wameumia vibaya.
“Tunashukuru
Mungu hakuna mtu amekufa hapa, lakini dereva wetu ameumia vibaya wamemchukua na
kumkimbiza Hospitali,” alisema Kambale.
Alisema
wakati yeye akiwa amewa amechoka baada ya kusafiri kwa siku mbili akitokea
Nairobi, alishtikia basi likiyumba kasha akasikia kishindo kikubwa na ndipo
alijikuta akitolewa kwenye gari hilo kupitia dirishani.
Daktari
Msaidizi wa Hospitali ya Misheni Chimala, Peter Seif Kigombola alisema kuwa
hospitali hiyo imepokea majeruhi 11, kati yao 10 walikuwa ji abiria wa basi la
Taqwa na mmoja alikuwa ni dereva wa lori aina ya Center.
Alisema
abiria hao tisa hali zao zinaendelea vizuri, lakini wawili ambao ni dereva wa
basi na kondakta wake hali zao ni mbaya na kuwa wamepewa rufaa ya kwenda katika
Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.
Alisema kuwa
dereva na kondakta wake walivunjika viungo mbalimbali vya miili yao kama vile
mikono na miguu na kupata majeraha mengine kichwani, hali ambayo imesababisha
hali zao kuwa mbaya.
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa
ajali hiyo na kusema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa
ajali hiyo pamoja na kukusanya taarifa
za majeruhi na kuwa atatoa taarifa ya ajali hiyo baadaye.
No comments:
Post a Comment