STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 11, 2013

JB amvulia kofia, King Majuto, Bi Hindu

Jacob Stephen 'JB'
http://www.timesfm.co.tz/content/accounts/38/uploads/cache/bi%20hindu_full.jpg
Bi Hindu

King  Majuto
MUIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini, Jacob Stephen 'JB' amemwagia sifa msanii mkongwe wa fani ya vichekesho, Amri Athuman 'King Majuto' na kudai ndiyo sababu inayomfanya arekodi naye filamu moja kila mwaka.
Alisema ucheshi wa King Majuto na umakini wake kazini, umekuwa ukimfanya mkongwe huyo kukosa mpinzani nchini na kuendelea kutamba licha ya umri kumtupa mkono.
"Sidhani kama kuna msanii wa kumzuia King Majuto, anajua kazi yake ndiyo maana nimejiwekea malengo kila mwaka niigize naye angalau filamu moja," alisema.
JB alisema King Majuto Majuto na Chuma Suleiman 'Bi Hindu' aliyewahi kung'ara na kundi la Kaole Sanaa ni miongoni mwa wasanii wanaomkosha ndiyo maana kila mara anaigiza nao na sasa amefanya nao kazi nayotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi huu.
"Wote wawili pamoja na Suleiman Barafu, Shamsa Ford watakuwepo kwenye filamu hiyo ya 'Shikamoo Mzee' na nitaendelea kuwashirikisha hata kwa kazi zangu nyingine wanapendeza na kunogesha filamu," alisema JB anayefahamika pia kama 'Bonge la Bwana'.
Kabla ya filamu ya Shikamoo Mzee, JB alicheza na King Majuto katika kazi iitwayo 'Nakwenda kwa Mwanangu' na aliingiza na Bi Hindu kwenye 'Zawadi Yangu' ambayo kwa sasa inaendelea kukimbiza sokoni.

No comments:

Post a Comment