STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 11, 2013

Man United, Bayern zitauana kwa Thiago

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyIG-FdMrwZIyQB3Fut8UQBMbFu5KYdfl2xFg59M8G-jWGIEitujeF3vD47t9lZVxoqC1uoJY4iiMcXBLMECvKIOI06aULU3hiXJfYb5mciLHll2GItkfAJBhyfqkoihC-MO8hhPWcT7on/s400/img-pas-de-jo-pour-thiago-alcantara-1341498767_620_400_crop_articles-159070.jpg
Thiago Alcantarra anayezitoa udenda Bavarian na Mashetani wekundu
 WAKATI kukiwa na tetesi kwamba dili la usajili wa nyota wa timu ya taifa ya Hispania U21 kwenda Manchester United limekamilika Bayern Munich wameibuka na kutangaza dhamira ya kumnyakua mchezaji na kuibua upinzani mkali juu ya Thiago Alcxantarra watu atatua katika ya klabu hizo mbili.
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola akizungumza na waandishi wa habari hii leo amesema kuwa anamfahamu vizuri Thiago na angependa kumsajili kwa kuwa ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya nne au tano .
Guardiola amesema kuwa kwa sasa mchezaji ambaye angependa kumsajili ni Thiaggo na kama hataweza kushawishi kujiunga na Bayern basi hatasajili mchezaji mwingine . Kauli hii ya Guardiola inamaanisha kuwa timu hizo mbili za United na Bayern kwa sasa zitakuwa zikihaha kila moja ikijaribu kumshawishi nyota huyo kusaini kwenye  timu mojawapo.
United imekuwa ikitajwa kujiandaa kumtangaza mchezaji huyo kama mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa kusajiliwa na David  Moyes baada ya usajili wa beki wa Uruguay Guillermo Varella na kiungo huyo (Thiago) amekuwa akijaribu kuondoka Barcelona alikoshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza .
Thiago Alcantarra ana malengo ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazil mwakani na amekuwa akipambana kuondoka Barcelona ili aende mahali ambako atamshawishi kocha Vicente Del Bosque kumpa nafasi . Mkataba wa Alcantara unaonyesha kuwa asipocheza kwenye asilimia 60% ya mechi za timu hiyo anaweza kuuzwa kwa bei ya Euro Milioni 18 na kwa msimu uliopita hakucheza kwa kiwango hicho hali inayofanya kuondoka kwake kuwa rahisi .

No comments:

Post a Comment