Benson Mwakyembe |
Mada Maugo (kulia) akiwa na Rais wa TPBO-Limited Yasin Abdallah 'Ustaadh' |
Kwa mujibu wa Rais wa TPBO-Limited, Yasin Abdallah 'Ustaadh' mabondia hao wataondoka Julai 23 ambapo Maugo ataenda kupigana na Movsur Yusupov wakati Mwakyembe yeye ataonyeshana kazi na Apti Ustarkhanov kwenye michezo itakayochezwa kwenye ukumbi wa Trade & Intertainment uliopo mji wa Kasiysk, nchini Russia.
Ustaadh alisema watanzania hao watapigana na Warusi hao katika michezo ya kilo 75 (Super Middle Weight) itakayokuwa na raundi nane kila mmoja.Rais huyo wa TPBO alisema mpinzani wa Maugo rekodi yake inaonyesha kuwa amecheza mapambano matatu na yote ameshindwa moja likiwa kwa KO wakati mpinzani wa Mwakyemba amecheza mechi mbili na kushinda moja na mwingine kupigwa.
"Pamoja na rekodi ndogo za wapinzani wao, lakini ikumbukwe kuwa mabondia wa Russia na kwingineko Ulaya huwa hawachezi ngumi za kulipwa bila kucheza ngumi za ridhaa na kufikia hatua ya kushiriki michuano ya Olimpiki kwa maana hiyo Maugo na Mwakyembe wakitarajiwe wepesi Russia," alisema Ustaadh.
Ustaadh aliongeza kuwa tayari mabondia hao wa Tanzania wameshaombewa visa za kwenda nchini humo gharama zote zikilipwa na TPBO-Limited na wataondoka nchini wakiongoza na wakala wao kutoka Kenya, Thomas Mutua atakayeondokea Kenya na kukutana na mabondia hao Dubai.
No comments:
Post a Comment