MSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule 'Profesa Jay wa Mitulinga' amepatwa na msiba mkubwa naada ya mama yake mzazi kufariki usiku wa kuamkia leo baada ya kugongwa na gari eneo la Mbezi Juu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana usiku wa kuamkia leo ni kwamba bi mkubwa huyo anayefahamika kwa jina la Rosemary Majanjara Haule aligongwa na gari lisilofahamika wakati akivuka barabara kuelekea dukani majira ya saa 2 na kupoteza uhai alipokuwa akiwahishwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
MICHARAZO inampa pole Profesa Jay, Black Rhyno na ndugu jamaa na rafiki wa familia ya Haule kwa msiba huo mzito ambao umefululiza kwa wasanii kuondokewa na wazazi baada ya Barnabas kumpoteza mama yake kabla ya majuzi Z Anto.
No comments:
Post a Comment