STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 14, 2014

Yanga ya Maximo kiwangoo! yaiua Azam x3

Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka Erasto Nyoni wa azam (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto )
Kikosi cha Azam kilichozimwa Taifa leo
Kikosi ch Yanga kilichotwaa Ngao ya Hisani leo kwa kuilzaza Azam
 KLABU ya Yanga iliyo chini ya kocha Marcio Maximo wa Brazil, jioni ya leo imetuma salamu kwa klabu nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifumua bila huruma watetezi wa ligi hiyo, Azam mabao 3-0 katika pambano la Ngao ya Hisani lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Yanga ikiwa katika kiwango cha juu na kuwafunika wapinzani wao, walithibitisha kuwa bado ni wababe wa Azam katika mechi ya Ngao ya Hisani baada ya kuifdunga kwa msimu wa pili mfululizo kwani msimu uliopita waliitambia kwa bao 1-0.
Mabao yaliyoizamisha Azam waliotwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita bila ya kupoteza mchezo wowote yalitumbikizwa wavuni na Gelinson Santana 'Jaja' aliyefunga mabao mawili na kuzima ngebe za mashabiki waliokuwa wakimzomea kabla ya Simon Msuva kufunga jingine akitokea benchi kumpokea Nizar Khalfan.
Kipigo hicho cha Azam kimevunja rekodi ya kocha Joseph Omog pamoja na vijana wao ambao walikuwa wakifurahia kushinda au kutoka sare bila kupoteza mchezo wowote tangu mwaka jana katika mashindano nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment