STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 14, 2014

Nyatawe 'awafunda' wenzake, ataka wajiheshimu

MUIGIZAJI mahiri wa filamu nchini aliyewahi kutamba na makundi ya Shirikisho Msanii Afrika, Happy Mkamwa 'Nyatawe' amewataka wasanii wenzake wa kike kupenda kujiheshimu na kujithamini ili nao waheshimiwa na kuthaminiwa na jamii.
Aidha aliwataka wasanii nchini kwa ujumla kuwa wabunifu na kuumiza vichwa ili kutoa kazi ambazo zitabamba anga la kimataifa.
Akizungumza na MICHARAZO, Nyatawe alisema wasanii wa kike wanapaswa kujitambua wao ni  nani ndani ya jamii na hivyo kuwa mfano bora kuanzia mavazi yao, matendo na hata kwa kauli zao ili kujijengea heshima mbele ya jamii inayowazunguka.
Alisema kuendelea kufanya mambo ya ovyo yanawashushia heshima na kufanya wadharaulike.
"Wasanii wa kike wa leo ndiyo wazazi na walezi wa kesho wa familia hivyo ni wajibu wetu kuwa makini kwa kila tunalofanya au kulitamka, ili kujenga heshima na hadhi zetu," alisema.
Pia aliwakumbusha wasanii kupenda kuwa wabunifu katika kazi zao pamoja na kujituma kwa bidii ili mwishowe waje kutamba kimataifa badala ya kuridhika na mafanikio ya nyumbani.

No comments:

Post a Comment