NAHODHA wa Chelsea John Terry amemuunga mkono Jose Mourinho kufanikiwa kwenye
Klabu yake mpya Manchester United huku akimueleza kuwa Meneja huyo ndie
bora kupita yeyote aliewahi kucheza chini yake. Terry alikaribia kuondoka Chelsea mwishoni mwa Msuimu huu baada ya Mkataba wake kumalizika lakini sasa ameongezewa Mwaka Mmoja na Msimu ujao atakuwa chini ya Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte ambae ni Meneja wa sasa wa Timu ya Taifa ya Italy.

No comments:
Post a Comment