STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 30, 2016

Samatta aweka rekodi Ulaya aibeba Genk

Samatta-ushindi 
We're going to Europe!STRAIKA Mbwana Samatta amweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuiwezesha timu yake kucheza michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya (UEFA Europa League) baada ya kuisaidia Genk ya Ubelgiji kufuzu hatua hiyo kwa kuilaza Charleroi.
Genk iliyopoteza mchezo wa kwanza katikati ya wiki iliyopita kwa mabao 2-0 ugenini iliikandika Sporting Charleroi kwa mabao 5-1.
Samatta aliyeanza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ikiwa mechi yake ya 18 tangu alipojiunga na timu hiyo kutoka TP Mazembe ya DR Congo, aliibeba timu yake hiyo katika mechi hiyo ya Uwanja wa nyumbani wa Cristal Arena.
Mkali huyo na nahodha wa Taifa Stars, alifunga bao moja ambalo lilikuwa ni goli la pili kwenye mchezo huo, huku Mgiriki Nikolaos Karelis akifunga hat-trick akianza na Mkwaju wa penalti dakika ya 17, kisha Samatta akazamisha bao la pili dakika ya 27 kabla ya Sandy Walsh kupiga bao la tatu dakika ya 45.
Kipindi cha pili Genk waliongeza mabao mengine mawili kupitia Karelis aliyefunga bao la nne dakika ya 56 kisha kukamilisha hat-trick yake dakika ya 71 kwa kufunga bao la tano.
Genk imefuzu kucheza michuano ya Europa ligi kwa matokeo ya jumla 5-3 na itaanzia hatua ya awali ya mtoano kabla ya kuingia makundi iwapo itaing'oa timu itakayocheza nao hatua hiyo ya awali ya mtoano.

No comments:

Post a Comment