STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 9, 2014

Baby Madaha atoa mpya Kenya, awalilia akina Recho

NYOTA wa muziki za kizazi kipya na filamu aliyejichimbia nchini Kenya, Baby Madaha, amefyatua wimbo mpya uitwao 'Nawaponda' huku akiomboleza vifo mfululizo vya wasanii na wadau wa sanaa nchini.
Baby anayefanya kazi chini ya kampuni ya Cindy N' Cindy, aliliambia MICHARAZO kutoka Kenya kwamba wimbo huo tayari upo hewani kupitia vituo vya redio na mitandao ya kijamii.
Mwanadada huyo aliyeibuliwa kwenye ulimwengu wa sanaa kupitia shindano la BSS, alisema wimbo huo ameutoa 'audio' na video yake na kwamba ni muendelezo wake wa kuwapa burudani mashabiki wa muziki Afrika Mashariki na Kati.
"Nimeachia ngoma mpya ya 'Nawaponda' ambapo video yake tayari inachezwa hewani kupitia vituo vya runinga na mitandao ya kijamii," alisema.
Aliongeza kuwa, ameshtusha na taarifa ya misiba mfululizo ya wasanii na wadau wa filamu nchini na kusema anawapa pole wote walioguswa na misiba hiyo kwa namna moja au nyingine.
"Inasikitisha na vigumu kuamini kuwa ndani ya mwezi mmoja wana familia ya sanaa tumepoteza watu karibu wanne, inauma na ninawapa pole walioumizwa na misiba hii, hii ni kazi ya Mungu, tusichoke kumuomba kutupa nusura," alisema.
Wasanii waliofariki katika kipindi hicho kifupi ni Amina Ngaluma 'Japanese'. Adam Kuambiana, Rachel Haule 'Recho', mtayarishaji na muongozaji wa filamu na vipindi vya runinga, George 'Tyson' Otieno na mchekeshaji Said wa Ngamba 'Mzee Small'..

No comments:

Post a Comment