STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 9, 2014

Golden Bush kupeleka ujuzi wao Makambako

Kikosi cha Golden Bush Veterani
Benchi la ufundi la klabu hiyo likiongozwa na atakayekuwa mkuu wa msafara, Wazir Mahadhi, Madaraka Suleiman na Godfrey Chambua
WAKALI wa soka la maveterani, Golden Bush inatarajiwa kwenda mjini Makamabno kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki na wenyeji wao, Makambako Veterani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico', inasema kuwa mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Juni 22 kupimana ubavu na wazee wenzao wa huko, huku wakitamba kuwa wanaenda kugawa 'dozi' kama kawaida wanavyofanya jijini Dar na hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Ebu tiririka na taarifa hiyo ya Ticotico kama ilivyo hapo chini;

Tunapenda kutoa taarifa kwamba ile timu tishio upande wa veterans hapa nchini yaani Golden bush veterans ambao ndio mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani Bara na visiwani watakuwa Makamboko siku ya tarehe 22 June 2014 kwa mualiko wa Makambako Veterans wakishirikiana na Serengeti Breweries. Mwaliko huu umetokana na historia ndefu ya timu yetu ambayo imejijengea heshima ya kuwa na ushirikiano wa karibu na timu nyingi za veterans wakiwemo Makambako Veterans ambao ndio watakuwa wenyeji wetu siku ya tarehe 22. Aidha tunapenda kutumia nafasi hii kama sehemu mojawapo ya kutengeneza urafiki wa karibu Zaidi na timu za nyanda za juu kusini.

Maandalizi yamekamilika kwa asimia 95 ambapo mkuu wetu wa msafara bwana Waziri Mahadhi Mandieta akishirikiana na mwenyekiti wa kamati ya ufundi bwana Yahaya Issa wanakamilisha baadhi ya mambo madogo madogo tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Njombe.

Kesho tutakuwa na mechi ya kirafika na Wizara ya afya ikiwa na sehemu mahususi kabisa ya kupasha misuli kabla ya kuanza safari ndefu kabisa ya kuelekea Makambako. Karibuni sana, game ya kesho itapigwa katika uwanja wa Kinesi ali maarufu kama St James’ park kuanzia saa saa mbili kamili asubuhi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Onesmo Waziri “Man of the match” “Ticotico” “player Maker” Msemaji wa timu na Mchezaji Mwandamizi.
 

No comments:

Post a Comment