|
Rais Kikwete akishiriki kwenye dua ya kuuombea mwili wa Mzee Small nyumbani kwa marehemu |
|
Rais wa TAFF, Simon Mwakifamba akiwa na Juma Mbizo |
|
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere akiwa na Mkwere Original |
|
Wazee wa Mizengwe walikuwapo |
|
Mbembe akilia huku akitulizwa na Mafumu BIlal 'Bombega' |
|
Wazee walikuwa makini kuhakikisha hali ya usalama |
|
Kitwana Manara akiwa na wadau wenzake wa sanaa kwenye msiba huo |
|
Nyota wa filamu, Shamsa Ford, Deo Shija, Cathy na Sandra nao walikuwapo |
|
Issa Kipemba naye alikuwapo |
|
Mashaka aliyeipa kamera mgondo akiteta jambo na Steve Nyerere na MC, Mkwere Original |
|
Ramsey akiteta jambo na Niva |
|
Mama Abdul na waombolezaji wengine |
|
Mzee JKengua na Mzee Jangala walikuwapo bega kwa bega kwenye msiba huo |
|
Maskini mzee wetu tangulia 'ticha' sisi tu nyuma yako |
|
Shamsa Ford na wenzake |
|
Masheikh wakiendesha kisomo kumuombea Mzee Small katika safari yake ya Ahera |
|
Mtoto wa Marehemu, Muhidini Said |
|
JB akiwa na George Kayanda |
|
JB akihojiwa na wanahabari |
|
Pole sana kijana, Rais Kikwete akiteta na mtoto wa marehemu Mzee Small |
|
Rais akisaini kitabu cha maombolezo |
|
Rais Kikwete akiteta na Rais wa TAFF, Simon Mwakifamba |
|
Mzee Jangala akihojhiwa |
|
Richie naye akihojiwa na Saida Mwilima wa Star TV |
|
Mwili ukiombewa dua baada ya kuswaliwa |
|
Mwili ukiswaliwa swala ya Jeneza kabla ya kupelekwa kuzikwa |
|
Mtoto wa marehemu akisoma wasifu wa marehemu |
|
Wazee wa Ze Comedy Show nao walikuiwapo |
|
Safari ya kwenda kuzikwa inanza |
|
Add caption |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete leo amewaongoza maelfu ya waombolezaji waliojitokeza kumsindikiza kwenye makazi ya milele aliyekuwa mchekeshaji maarufu na mkongwe nchini, Said Ngamba 'Mzee Small'.
Rais Kikwete aliwaongoza waombolezaji hao waliojitokeza nyumbani kwa marehemu Mzee Small, Tabata Kisiwani jijini Dar es Salaam wakiwamo wasanii mbalimbali nyota na wanamuziki majira ya mchana wakati wa kisomo cha kumrehemu marehemu kabla mwili wake haujaenda kuzikwa jioni.
Rais Kikwete alipokewa kwenye msiba huo na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Nyerere na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani kwenda kumpa pole mjane wa marehemu.
Baada ya robo saa alitoka na kwenda kuungana na waombolezaji wengine kwa kutia saini kitabu cha rambirambi kabla ya kuteta na mtoto wa marehemu Muhidini Said na kumkabidhi bahasha yenye risala yake na kisha kuondoka msibani hapo.
Mbali na Rais Kikwete, Rais wa TAFF na Mwenyekiti wa Bongo Movie, msiba huo ulihudhuriwa na nyota mbalimbali wa fani ya sanaa wakiwamo wacheza filamu kama JB, Richie, Dk Cheni, Shamsa Ford, Deoi Shija, Niva, Nova, Slim Omar, Mzee Chillo, Mzee Jangala, Sandra na wengine.
Miongoni mwa wanamuziki waliokuwepo kwenye msiba huo ni pamoja na Roman Mng'ande 'Romario' wa Msondo Ngoma, Cosmas Chidumule, Mafumu Bilal 'Bombenga' na waigizaji waliowahi kufanya kazi na marehemu enzi za uhai wake pamoja na Rais wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher'.
Baadhi ya wasanii akiwemo Steve Nyerere na Mzee Jangala waliuelezea msiba huo kuwa ni pigo kubwa siyo kwa familia ya marehemu bali wasanii wote kutokana na ukweli Mzee Small alikuwa mmoja wa waasisi wa michezo ya kwenye runinga na mkongwe aliyewasaidia vijana wengi akiwa kama mwalimu.
Pia walisema kifo cha Mzee Small umekuja kuwatonesha donda ambalo bado halijapona la kuondokewa na wasanii mfululizo ndani ya muda wa mwezi mmoja sasa.
HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Marehemu
Mzee Small alizaliwa mwaka 1955. Alipata elimu ya msingi katika Shule
ya Msingi Mingumbi, Kilwa mkoani Lindi.
Mbali na ukongwe, Mzee Small
kila alipozungumza na watu hakuona sababu ya kuficha kusema yeye ndiye
msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.?
Mzee Small
alianza sanaa hiyo miaka ya sabini akifundishwa na mwigizaji Said Seif
‘Unono’ ambaye ni marehemu kwa sasa.
Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, Mzee Small ametumika katika vikundi vya mashirika mbalimbali nchini.
Marehemu
kila alipotajiwa Bi. Chau alisema ni mkewe wa ndoa wa kwenye maigizo
kauli ambayo wengi hawakuiamini wakijua anakwepa kumtambulisha moja kwa
moja.
Kuna wakati
mke wake, Fatuma Ngamba aliwahi kusema kwamba, hana wivu na Bi. Chau kwa
vile anajua anaigiza na marehemu na ndiyo kazi inayowafanya waishi.Katika kipindi cha mateso ya ugonjwa
wake, wadau mbalimbali walijitokeza kumsaidia kwa hali na mali huku wito
mkubwa ukitolewa kwamba, watu zaidi wajitokeze badala ya kusubiri kutoa
rambirambi.
Mzee Stori alianza kuigiza mwaka 1980 na kupitia makundi kadha kabla ya kuanzisha lake liitwalo Afro Dance.
Ameacha mjane na watoto sita pamoja na wajukuu saba.
Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu Mzee Small. Amina.
No comments:
Post a Comment