
Tuzio hizo zilitolewa mara baada ya mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu kati yao ya Polisi Moro ambapo Mbeya iliibuka washindi wa bao 1-0.
Kwenye tuzo hizo Kocha mkuu Juma Mwambusi alipata tuzo kama kocha mwenye mafanikio makubwa ndani ya kikosi cha city na ligi kwa ujumla Paul Nonga, Deus Kaseke, Themi Felix walipata tuzo ya heshima kwa kufanya vizuri misimu miwili Rafael Alfa na Kenny Ally walipata tuzo ya wachezaji chipukizi waliofanikiwa Haningtony Kalyusubula alipata tuzo ya mlinda lango bora na Juma Nyosso, Hassan Mwasapili na Peter Mwalyanzi walipata tuzo ya uchezaji bora

Halikadhalika wachezaji wengine 18 nao walipata zawadi ikumbukwe kuwa zawadi na tuzo hizo walizopata wachezaji wa City zimeambatana na bahasha iliyonona vizuri kutoka uongozi na mashabiki wa Mccfc.
No comments:
Post a Comment