STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 10, 2015

Ozil arejea Arsenal, Rojo, Blind waipa furaha Man Utd

Kipa Valdes akiwa na wachezaji wenzake wapya wa Manchester United

Daley Blind akifanya mazoezi hapa akiwa na Dogo Andreas Pereira
Rojo naye alipasha na wenzake
WAKATI Manchester United wakichelekea kurejea tena dimbani kwa nyota wake Marcos Rojo na Daley Blind, Kiungo Mesut Ozil wa Arsenal naye amepona na huenda akarejea uwanjani kesho wakati Arsenal inakipiga dhidi ya Stoke City.
Mashetani Wekundu wanatarajiwa kuwa nyumbani kuwavaa Southampton baada ya kupata sare mbili mfululizo ugenini katika Ligi Kuu ya England, lakini ikiwa na furaha kurejea kwa nyota hao sambamba na kumnasa kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes waliyemsainisha.
Kama ilivyo kwa Manchester, Arsenal wenyewe wanafurahi baada ya Ozil kurejea Ligi Kuu England baada ya kukaa nje miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti.
Kocha Arsene Wenger amesema Ozil amekuwa akifanya mazoezi na wenzake na sasa yuko fiti, hata hivyo inaonekana ataanzia benchi.
Mjerumani huyo aliyejiunga na Arsenal akitokea Madrid aliumia katika mechi dhidi ya Chelsea, Oktoba mwaka jana.
Ozil ndiye mchezaji ghali zaidi Arsenal iliyompata kwa kitita cha pauni milioni 42.5.

No comments:

Post a Comment