STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 11, 2015

Arsenal yaitoa nishai Stoke City Sanchez azidi kung'ara

The Arsenal players join star man Sanchez in celebration of his second goal of the afternoon
Wachezaji wa Arsenal wakipongezana
Arsenal defender Koscielny (6) heads the north London club into an early lead at the Emirates after just six minutes
Laurent Koscielny akifunga bao la kwanza la Arsenal kwa kichwa
MABAO mawili kutoka kwa Alexis Sanchez na jingine la beki Laurent Koscielny yameiwezesha Arsenal kupata ushindi mujarabu nyumbani dhidi ya 'wagumu' Stoke City katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya England.
Ushindi  huo umekuja wakati Arsenal ikitoka kupokea kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Southampton, ambapo kiungo Mesut Ozil, alirejea uwanjani katika pambano hilo la Emirates baada ya kuwa nje miezi mitatu.
Wenyeji walianza kuandika bao dakika ya 6 kupitia Koscielny kabla ya Sanchez kuongeza la pili dakika ya 33 na kuja kuongeza jingine dakika nne tangu kuanza kwa kipindi cha pili.
Katika pambano hilo Arsenal ilijikuta ikimpoteza beki wake Mathieu Debuchy aliyeumia bega mapema na nafasi yake kuchukuliwa na Bellerin dakika chache baada ya Koscielny kufunga bao la kuongoza kwa kichwa akimaliza krosi ya Sanchez ambaye kwa mabao mawili ya leo amefikisha mabao 12 katika ligi hiyo anayoicheza kwa msimu wa kwanza.

Kwa ushindi hio Arsenal imefikisha pointi 36 na kulingana na Southampton na kukamata nafasi ya tano wakati wapinzani wao wamesaliwa na pointi26 na kusalia kwenye nafasi ya 11.
Muda mchache ujao Manchester United watakuwa uwanja wa Old Trafford kupepetana na Southampton katika mechi nyingine ya ligi hiyo ambayo baadhi ya nyota wa Man Utd waliokuwa nje kwa majeraha watarejea dimbani.
Wachezaji hao ni Daley Blind na Angel di Maria  ambao wapo kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Louis Van Gaal.


No comments:

Post a Comment