STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 8, 2014

Fabregas afunguka ya moyoni kuhusu Chelsea

http://e1.365dm.com/14/07/800x600/Fabregas_3179732.jpg?20140728165853
Sikuwahi kuota kuja kuzaa uzi wa Chelsea kabisa aisee....dunia inabadilika sana
CESC Fabregas amekiri kwamba hakuwahi kufikiria hata mara moja kama angekuja kuitumikia klabu yake ya sasa ya Chelsea.
Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona, alisema wazo la kuitumikia klabu hiyo chini ya Jose Mourinho lilikuwa halifikiriki katika kipindi cha nyuma. 
Fabregas aliyerejea tena kwenye Ligi Kuu katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi baada ya kushindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Barcelona, alisema kama mtu angemuambia miaka mitano nyuma kwamba atakwenda kucheza Chelsea chini Mourinho ni jambo ambalo asingeamini lakini maisha yanabadilika. 
Kiungo huyo alidai alianza kufikiria kuondoka Barcelona baada ya fainali ya Kombe la Mfalme ambayo walifungwa na Real Madrid ambapo baada ya kuzungumza na mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta aliona kama amewapunguzia bugudha kutokana na kauli yake. 
Baada ya hapo alimuomba wakala wake amtafutie timu nyingine na Chelsea wakatoa ofa ambapo baada ya kuzungumza na Mourinho na kumwambia mambo anayohitaji akaona hapo ndio patakapomfaa.

No comments:

Post a Comment