STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 8, 2014

Polisi Geita wanasa wawili, bunduki 7 mabomu 10

Bunduki 7 na mabomu 10  yaliyokamatwa huko Bukombe

MSAKO mkali unaoendelea Geita kusaka wale wote waliohusika na tukio la kuvamiwa na kisha kuuwawa kwa askari Polisi wawili wa kituo cha Polisi cha Bukombe, umefanikiwa kuwanasa wawili na silaha kadhaa yakiwamo mabomu.
Habari zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Geita ni kwambawatu wawili walikamatwa na kukutwa na bunduki saba na mabomu 10 eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe.

Inasadikiwa kuwa bunduki hizo ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu  usiku wa kuamkia juzi na kujeruhi askari wawili.

Tunaarifiwa kuwa Bunduki zilizokamatwa nne ni SMG na tatu aina ya Shotgun  pamoja na panga zimepatikana  katika tanuru la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.

Habari zinasema kuwa  katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi linaloendelea kufanya kazi nzuri  limekamata watu watatu  pia  na mwalimu mmoja wa shule ya sekondari Ushirombo anayedaiwa kushiriki katika tukio.
Msako huo wa jeshi la polisi bado unaendelea kufanya msako mkali ili kuwakamata wahusika wote na silaha zote zilizoporwa na majambazi.

No comments:

Post a Comment