STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 7, 2014

Malawi yapigwa 2-0 na Mali ugenini Afrika

http://www.malawidemocrat.com/wp-content/uploads/2012/06/Flames-e1339493490888.jpg
Kikosi cha Malawi kilichonyolewa 2-0 ugenini leo
TIMU ya taifa ya Malawi imekumbana na kipigo cha mabao 2-0 ugenini mbele ya wenyeji wao Mali katika mechi ya kiporo cha mechi za makundi za kuwania kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.
Mechi hiyo ya kundi B ilishindwa kufanyika jana kama ratiba ilivyokuwa ikionyesha kutokana na mvua kubwa iliyopiga katika mji wa Bamako na kusogezwa mpaka leo.
WEnyeji walitumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kuwanyoosha The Flames kwa mabao 2-0 na hivyo kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu sawa na Algeria iliyoinyoa Ethiopia kwa mabao 2-1, ila Mali wanaongoza kwa uwiano wa mabao ya kufungwa na kufungwa.

No comments:

Post a Comment