STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 7, 2014

DRFA yafanya madudu, mechi ya Big Bullets Yanga yaota mbawa

http://news.maraviexpress.com/wp-content/uploads/2014/05/Bullets.jpg
Big Bullets iliyokwama kuja jijini kucheza na Yanga
http://2.bp.blogspot.com/-eS9TrOZN3qw/T-8WW5gQF2I/AAAAAAAAIfs/lb4M1UdjOO4/s1600/Yanga+express+2.jpg
Yanga walioikosa Big Bullets
PAMBANO la kirafiki la kimataifa baina ya Yanga na Big Bullets ya Malawi, limeota mbawa baada ya timu hiyo iliyokuwa ikielezwa ilikuwa Mbeya kushindwa kutua nchini na kusababisha usumbufu mkubwa kwa mashabiki wa kandanda waliofurika uwanja wa Taifa kwenda kushuhudia mechi hiyo.
Inaelezwa kuwa timu hiyo wala haikuwa nchini kama ilivyokuwa imetangazwa awali na kwamba ujio wake chini ya ufadhili wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na badala yake ilikuwa kwao Malawi ikishuka dimbani leo kucheza mechi ya ligi ya nchi yao.
Yanga ilikuwa imeupania mchezo huo ambao ungekuwa wa mwisho kwao kabla ya kuivaa Azam kwenye mechi ya Ngao ya Hisani Jumapili ijayo kwenye uwanja huo huo wa Taifa kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara 2014-2015.
Viongozi wa DRFA hawakupatikana kueleza kilichotokea katima ujio wa Big Bullets inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya nchi yao, huku viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya wakidai timu hiyo haikuwa mjini humo na waliitegemea baada ya kucheza na Yanga ndiyo ingetua jijini humo kucheaa mechi na Mbeya City.

No comments:

Post a Comment