Vijana kama hawa wanapaswa kuamka kupigania haki zao |
Suleiman Msuya
VIJANA wametakiwa kuwa na ushirkiano ili kuhakikisha
kuwa Baraza la Vijana linatambulika katika Katiba ambayo itapatikana kwani
kutawajengea kupata fursa za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kitamaduni.
Rai hiyo imetolewa na vijana wenzao Humphrey
Polepole, John Mnyika, Paul Makonda na Maria Sarungi ambao walikuwa katika
kongamano lilioandaliwa na Shirika la Tanzania Youth Vision Association (TYVA)
kwa kushirikiana na Umoja wa Azaki za vijana mbalimbali.
Watoa mada hao kwa pamoja walionekana kusisitiza
uwepo wa ushirikiano baina yao bila kujali dini, itikadi za vyama na sifa
zingine za uongozi kwa lengo la kutetea haki za vijana wa leo na kesho wa
Tanzania.
Akizungumza katika kongamano hilo aliyewahi kuwa
Mjumbe wa Tume ya Rasimu ya Katiba Hamphrey PolePole alisema pamoja na kuwa na
msimamo na ushirkiano ni vema vijana wakahoji ni kwa nini Zanzibar inatengeza
sheria dhidi ya baraza la vijana wakati rasimu inayojadiliwa kwa sasa imetaja
baraza hilo.
PolePole alisema ni wazi kuwa vijana wa Tanzania
hasa Tanzania Bara wanahitaji ila jambo la msingi ni kuangalia kwa makini kwa
kusoma rasimu vizuri ili waweze kujianda kifkra iwapo rasimu hiyo itapita kuwa
itafanya kazi katika mazingira gani.
“Nashukuru kupata nafasi hii ila ni vema kila kila
kijana wa Tanzania Bara akajiuliza ni kwa nini Zanzibar inatengeneza sheria
yake wakati inatambua kuwa rasimu imeweka kipengele hicho katika ibara ya 44 ya
rasimu”, alisema
Naye Mbunge wa Bunge la Katiba John Mnyika aliwataka
vijana kupigania haki zao ila akawataka kujiandaa pia kwa kutokuwepo kwa katiba
kwani kinachoendelea huko Dodoma ni uchakachuaji wa rasimu iliyopendekezwa na
Tume ya Katiba.
Kwa upande wake Maria Sarungi aliwataka vijana
kujifunza uvumilivu na kuheshimiana pamoja na kuzingatia demokrasia kwani bila
kufanya hivyo hata hayo ambayo wanayalilia yanaweza yasiwe na tija kwa na kwa
Taifa.
Aidha Sarungi aliomba vijana kuhakikisha kuwa haki
ya ubunifu inatambulika kikatiba kwa kuzingatia kuwa iwapo wabunifu
watatambulika kikatiba watapata maendeleo kama walivyofanikiwa watu mbalimbali
akimtolea mfano tajiri wa kimarekani Bill Gates.
Akizungumza katika kongamano hilo Paul Makonda
ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Katiba alisisitiza iwapo suala la kuwepo kwa
Baraza la Vijana kutazingatia mitazamo ya vyava ni wazi kuwa vijana wengi ambao
hawana uhusiano na vyama hawatakuwa tayari kujiunga na kushiriki.
Makonda aliwataka vijana kuacha kutumika katika sula
hilo kwa kile alichodai kuwa wahitaji wakubwa ni wao na ni wajibu wao kupigania
uwepo wake kwa kutumia njia sahihi ili kuepusha migongano.
No comments:
Post a Comment