STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 7, 2014

Loic Remy achekelea kuwa Chelsea, lakini...!

Delight: Remy signed for Chelsea on final week of the transfer windowMSHAMBULIAJI wa Chelsea,  Loic Remy amesema bado haelewi kwanini dili la kujiunga na Liverpool majira ya kiangazi lilivunjika.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alitazamiwa kujiunga Anfield kwa dau la paundi milioni 8 kabla ya wekundu hao kulitupilia mbali dili hilo wakidai mchezaji huyo ameshindwa kufuzu vipimo vya afya.
Remy alishindwa kufuzu vipimo vya afya kutokana na matatizo ya moyo na goti, lakini alishangazwa na tangazo hilo.
“Binafsi sikuelewa. Tatizo wakati wa vipimo vya afya? sijui. Walitengenezea, lazima itakuwa hivyo,” aliwaambia Daily Star.
Mfaransa huyo alirejea QPR na alionekana katika mechi ya ligi kuu kabla ya kujiunga na Chelsea wiki ya mwisho ya usajili ambapo atacheza kumsaidia Diego Costa ambaye amepata majeraha ya nyama za paja katika majukumu ya kimataifa.

Remy, ambaye aliifungia Ufaransa bao la ushindi dhidi ya Hispania siku ya alhamisi, alisema; “Kichwani mwangu, nilitaka kuendelea kukaa QPR, lakini sikuogopa kwa sababu nyingi  nilizonazo: Kwa jinsi nilivyojiimarisha, kujiamini kwangu na kwa namna Chelsea walivyonihitaji, nilikubali kwasababu hii ni moja ya klabu kubwa duniani.
“Nina furaha ya kujiunga na klabu hii”

No comments:

Post a Comment