STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 7, 2014

Yanga kuivaa Big Bullets bila Cannavaro, Ngassa Taifa leo

http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/07/andrew-coutinho1.jpg
Yanga walipokuwa wakijifua ufukweni
YANGA itacheza mchezo wake wa mwisho wa kujipima ngumu kwa kuvaana na Big Bullets ya Malawi katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa uwanja wa Taifa.
Hiyo ni mechi ya tano kwa Yanga chini ya Marcio Maximo ikiwa haijapoteza mchezo wowote na wa pili wa kimataifa baada ya katikati ya wiki kuilaza Thika United ya Kenya.
Katika mechi hiyo ya leo ambayo itakuwa ya mwisho kabla kujichimbia kambini kujiandaa na mechi ya kuwania Ngao ya Hisani dhidi ya Azam Jumapili ijayo kwenye uwanja huo huo.
Yanga hata hivyo itawakosa baadhi ya nyota wake katika mchezo wa leo akiwamo Nahodha Nadir Haroub Cannavaro,Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa na Simon Msuva waliopo Burundi na kikosi cha Taifa Stars kinachocheza mechi ya kirafiki ya kimataifa leo mjini Bunjumbura.
Hata hivyo Yanga bado ina wakali wengine ambao waling'ara katika mechi yao iliyopita dhidi ya Thika akiwamo Andrey Coutinho kutoka Brazil.

No comments:

Post a Comment