STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 7, 2014

Simba wawararua Wakenya 3-0 Taifa

Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Mkenya Paul Kiongera akishangilia moja ya mabao yake mawili katika ushindi wa 3-0 jioni ya leo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Chini ni mashabiki wa timu hiyo wakifurahia raha za Kiongera, mkali mpya wa mabao wa Msimbazi.

Vigogo wa kundi la Friends Of Simba SC, kushoto Zacharia Hans Poppe kulia Crescentius Johm Magori wakila raha Taifa leo

Mtu hatari mbele ya lango; Paul Kiongera kushoto langoni mwa Gor Mahia leo

Kocha wa Yanga SC (picha ndogo chini kushoto), Marcio Maximo kulia akiwa Msaidizi wake, Mbrazil mwenzake, Leonardo Leiva wakifuatilia mchezo wa kirafiki kati ya Simba SC na Gor Mahia ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba imeshinda 3-0. picha kubwa ni wachezaji wa Simba wakishangilia moja ya mabao yao leo

AKIWA anaijua vyema timu yake ya zamani ya Gor Mahia ya Kenya, nyota mpya wa kimataifa wa Simba ya Dar es Salaam, Raphael Muigai Kiongera 'Modo' leo ameiongoza Simba kushinda goli 3-0  katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa jioni ya leo.

Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na nyota huyo aliyesajiliwa kutoka Gor mahia ya Kenya, Raphael Kiongera alkiingia kipindi cha pili akitokea benchi na bao moja kuwekwa wavuni na  Ramadhan Singano 'Messi'.

Simba imetoa kichapo hicho ikiongozwa na kocha wake wa mara ya tatu, Mzambia Patrick Phiri ambaye alikishusha kikosi hicho uwanja wa taifa jiji Dar es Salaam ikiwa ni takriban mwezi na siku kadhaa tangu ilipo pata kichapo cha goli 3-1 na kupelekea kutimuliwa kwa kocha Zdravko Logarusic kutoka kwa Zesco United.

Kiongera alipachika goli dakika ya 55 wakati goli la pili likifungwa dakika ya 74 na Messi na Kiongera tena kufunga hesabu katika dakika ya 78.
CRD: HABARI24

No comments:

Post a Comment