STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 7, 2014

Cameroon yaua ugenini, Nigeria yafa nyumbani Afrika

http://www.africaplays.com/uploads/v7w6v6p4.jpg
Nigeria hawaamini kama walefungwa nyumbani
http://www.spotonsport.com/img/video/dr-congo-vs-cameroon-06092014.png
Cameroon wakishingailia moja ya mabao yao mjini LUbumbashi
http://static.cameroonweb.com/GHP/img/pics/48838821.295.jpg
MABAO mawili kutoka kwa wachezaji chipukizi Clinton Njie na Vincent Aboubakar walitosha kuiwezesha Cameroon kuanza kampeni zao za kuwania kwenye katika Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kwa kuwalaza wenyeji wa DR Congo mjini Lubumbashi katika mechi ya kundi D.
Visiting Cameroon posited a 2-0 win over DR Congo in their Group D clash on Saturday in Lubumbashi.
Mabingwa hao wa mara nne wa Afrika walipata mabao hayo katika kila kipindi na kuwapa pointi tatu muhimu ugenini katika mechi hizo za kuwania kufuzu fainali za Morocco.
Katika mechi ya kundi A Nigeria ikiwa nyumbani ilianza vibaya kampeni zake za kutetea taji lake kwa kukubali kipigo cha mabao 3-2 toka kwa Congo Brazaville na kuungaana na Sudan walionyukwa mabao 3-0 nyumbani kwao na Afrika Kusini kuburuza mkia katika kundi hilo.
Katika kundi B mechi kati ya Mali na Malawi ilishindwa kufanyika jana na kuahirishwa mpaka leo kutokana na mvua kubwa, huku Algeria ikiwa ugenini ikipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Ethiopia.
Guinea ikiwa nyumbani iliishinda Togo mabao 2-1 katika mechi ya kundi E wakati Ghana ikiwa uwanja wa nyumbani ikilazimisha sare ya 1-1 na Uganda The Cranes.
Kundi C Burkina Faso iliinyoa Lesotho waliowafuata nyumbani kwaoi Ouagaoudougou na Gabon ikiilaza Angola kidude kimoja (1-0) katika mechi iliyochezwa uwanja wao wa nyumbani.
Katika mechi nyingine ya kundi D, Ivory Coast ikiwa nyumbani kwao iliisasambua majira zao Sierra Leone kwa mabao 2-1, huku katika mechi za kundi F Zambia ilitoshana nguvu na majirani zao Msumbiji kwa kutofungana na Cape Verde ikiwa ugenini iliisambaratisha Niger kwa mabao 3-1.
Mechi za kundi G, ilishuhudiwa Senegal ikiilaza Misri mabao 2-0 na  Tunisia ikiwa nyumbani ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wageni wao Botswana.
Kipute cha mechi hizo za makundi zitaendelea tena siku ya Jumatano kwa kushuhudia nchi mbalimbali zikionyeshana kazi kuwania fainali hizo za mwaka 2015 zinazosubiriwa kwa hamu ni zile za Misri dhidi ya Tunisia, Cameroon na Ivory Coast na Togo na Ghana.
Ratiba kamili ya siku hiyo ni kama ifuatavyo:

Kundi A
Rwanda     v   Sudan  
Afrika Kusini vs Nigeria
Kundi B
Malawi v Ethiopia
Algeria v Mali
Kundi C
Angola v Burkina Faso
Lesotho  v Gabon
Kundi D
Cameroon v Ivory Coast
Sierra Leone v DR Congo
Kundi E
Togo v Ghana
Uganda v Guinea
Kundi F
Cape Verde v Zambia
Msumbiji v Niger
Kundi G
Misri v  Tunisia
Botswana vs Senegal

No comments:

Post a Comment