STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 6, 2014

Arturo Vidal awajibu waliompakazia

http://www.101greatgoals.com/wp-content/uploads/2014/08/vidal3.jpgBAADA ya kupakaziwa kuwa ni majeruhi wa goti, Kiungo wa Juventus,  Arturo Vidal amejibu mapigo juu ya taarifa hiyo ya kupata majeraha  akiwa katika majukumu ya kimataifa na Chile.
Ripoti zilieleza kuwa Vidal, ambaye alihusishwa kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi mwaka huu, aliondoka mazoezini mjini Miami baada ya kuumia goti kwa mara nyingine.
Hata hivyo, Vidal kupitia akaunti yake ya Twitter amekanusha taarifa hizi akisema alikuwepo muda wote katika mazoezi ya timu hiyo.
“Goti langu liko sawa,” Vidal aliandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii. “Tafadhali acheni kuzusha taarifa. Njooni Chile”.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alifanyiwa upasuaji wa goti mwishoni mwa msimu uliopita na alionekana kutokuwa fiti sana katika fainali za kombe la dunia.
Majeruhi imemuathiri Vidal katika haraka zake za kujijenga kuwa miongoni mwa viungo bora wa dunia.

No comments:

Post a Comment