STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 6, 2014

Balotelli alizua Liverpool mechi ya kirafiki

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mario Balotelli alitolewa nje katika mchezo wa kirafiki ambao mashabiki hawakuhudhuria dhidi ya Wolves baada ya kuanza kuzozana na refa Chris Foy.

Balotelli, 24, aliyehamia Anfield kutoka AC Milan kwa Pauni Milioni 16 mwezi uliopita, alizuiwa na Kolo Toure wakati Foy akizungumza naye kwenye mchezo huo Melwood.

Chanzo cha mzozo huo ni baada ya Mtaliano huyo kugongana na mchezaji wa Wolves. Baada ya mzozo huo tu, Balotelli alitolewa nje mara moja.

Hana furaha: Kolo Toure (kushoto) akimzuia Balotelli asiendelee na mzozo

You're off! Balotelli walks towards the touchline after being immediately substituted following the incident
Balotelli akielekea nje baada ya mzozo huo
Toure aliweka bega lake kumdhibiti mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa Manchester City asiendelee kuzozana na Foy juu ya tukio hilo kabla ya Balotelli kutolewa aingie mchezaji mwingine.

Nyota huyo wa zamani wa Inter Milan alianza pamoja na wachezaji kama Adam Lallana, Jose Enrique na Lucas Liverpool ikishinda 1-0 dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza, bao pekee la Lallana.

In action: Balotelli attempts to take the ball around Wolves' goalkeeper during the behind closed doors game
Balotelli alichukua mpira kwenye himaya ya kipa wa Wolves katika mchezo huo


On the run: The former Manchester City striker bursts forward during Liverpool's 1-0 win

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City aliisumbua mno ngome ya Wolves katika mchezo huo

No comments:

Post a Comment