UONGOZI wa klabu ya Young
Africans Sports Club umeitisha mkutano mkuu wa wanachama wa mabadiliko
ya Katiba ili wanachama waweze kutoa maamuzi kwenye baadhi ya vipengele
vilivyoongezwa kabla ya kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa
viongozi.
Akiongea na waandishi wa habari
makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani, Katibu Mkuu wa Young Africans Bw
Beno Njovu amesema wamefikia kuitisha mkutano huo wa mabadiliko ya
Katiba ili wanachama wapate fursa ya kupitisha baadhi ya vipengele kabla
ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
“Tumekua na mawasiliano na TFF
juu ya kuongezwa baadhi ya vipengele kwenye Katiba yetu kabla ya kufanya
uchaguzi mkuu wa viongozi, baada ya hapo ni nafasi kwa wanachama wa
Yanga sasa kukutana na kuweza kupitisha hivyo vipengele vitakavyoongezwa
kwenye Katiba Mpya” alsiema Beno.
Aidha Beno amesema wanachama
wakishapitisha/kukubaliana juu ya hivyo vipengele ndipo uoungozi
utawasilisha mapendekezo hayo kwa TFF ambayo ikishayabariki,
yatapelekewa kwa Msajili nae akiyapitisha ndipo itakua tayari ni Katiba
halali ambayo itatumika kwwenye uchaguzi mkuu.
“Nawaomba wanachama wa Yanga
wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano wa mabadiliko juni mosi 2014 ili
waweze kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea kuwa na Katiba Mpya
itakayotumika kwa shughuli za kila siku za klabu ya Yanga SC” aliongea
Beno.
Eneo na Ukumbi utakapofanyika mkutano huo Juni Mosi 2014 utatangazwa hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika.
CHANZO: TOVUTI YA YANGA
No comments:
Post a Comment