KIUNGO
nyota chipukizi wa Simba, Said Ndemla amezitahadharisha klabu ambazo
zinamnyemelea kutopoteza muda wao kwa vile hana mpango wa kutimka
klabuni hapo.
Akizungumza na MICHARAZO, Ndemla alisema bado yupo sana Msimbazi, klabu iliyosaidia kukuza kipaji chake.
Ndemla
anayemudu nafasi zote za kati, alisema kwa sasa akili yake ni kujipanga
kwa msimu ujao kuhakikisha Simba inakuwa na mafanikio makubwa baada ya
msimu huu kupepesuka na kumaliza kwenye nafasi ya nne baada ya kipindi
kirefu.
"Bado
nipo sana Msimbazi, wanaonimezea mate wasipoteze muda wao kwani sina
mpango wowote wa kiondoka kwa sasa Simba, nafikiria jinsi ya kuisaidia
kwa msimu ujao ili turejeshe heshima mjini," alisema.
Kiungo
huyo aliyejijengea jina kubwa hasa katika pambano la watani wa jadi la
duru la kwanza lililoisha kwa sare ya 3-3 baada ya kuingia dimbani na
kufanikiwa kubadilisha matokeo ya timu yake kulala mabao 3-0 na kumaliza
kwa sare.
Ndemla
na William Lucian 'Gallas' waliingizwa dimbani kipindi cha pili
kuchukua nafasi za Abdulhalim Humud 'Gaucho' na Haruna Chanongo na
kufanikiwa kuwadhibiti Yanga na kurudisha maabao matatu kupitia kwa
Joseph Owino, Gilbert Kaze na Betram Mombeki.
Kauli
ya Ndemla ya kudai ataendelea kusalia Simba imekuwa kukiwa na tetesi
kwamba kiungo huyo anatolewa macho na baadhi ya klabu za Ligi Kuu kwa
ajili ya kunasa
saini yake ili kuzichezea msimu ujao.
No comments:
Post a Comment