STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, May 8, 2014

Kuziona Ngorongoro vs Nigeria Buku 2 tu

Ngorongoro Heroes itakayoikaribisha Nigeria siku ya Jumapili uwanja wa Taifa
MASHABIKI wa soka watalazimika kulia kiasi kidogocha Sh Elfu mbili tu ili kuweza kuishuhudia timu ya taifa ya vijana U20 Ngorongoro Heroes itakayoumana na vijana wenzao wa Nigeria 'Flying Eagles' silku ya Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kiingilio cha chini kabisa katika mtanange huo wa kuwania  tiketi ya Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kitakuwa Sh. 2,000.
Flying Eagles imewasili usiku wa kuamkia leo na msafara wa watu 32 kwa ndege ya Ethiopian Airlines ambapo imefikia hoteli ya Sapphire. Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itafanyika kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nigeria inayofundishwa na kocha Manu Garba itafanya mazoezi leo (Mei 8 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi siku ya Jumapili.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa ni sh. 5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika magari maalumu.
Ngorongoro Heroes ambayo katika raundi ya kwanza iliitoa Kenya kwa jumla ya mabao 4-3 inaendelea kujinoa jijini Dar es Salaam chini ya Kocha wake John Simkoko na Msaidizi wake Mohamed Ayoub kujiweka sawa kwa mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na washabiki wa mpira wa miguu nchini.
Nigeria kama ilivyo kwa nchi nyingine 12 imeanzia moja kwa moja raundi ya pili kutokana na ratiba iliyopangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Nchi hizo ni Afrika Kusini, Angola, Benin, Burkina Faso, Cameroon, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mali, Misri, Morocco na Zambia.

No comments:

Post a Comment