MICHUANO ya soka ya ufukweni (beach soccer) inayoendeshwa na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikishirikisha vyuo mbalimbali vya Dar es
Salaam imeingia hatua ya robo fainali.
Robo fainali hiyo inayoshirikisha timu nane itachezwa Jumamosi
(Mei 10 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni kuanzia saa 5
asubuhi, huku Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii
(SWI) zikicheza robo fainali ya kwanza.
Chuo Kikuu cha Ardhi (AU) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere watcaheza robo fainali ya pili kuanzia saa 6 kamili. Saa 8 kamili
itaanza robo fainali ya tatu itakayozikutanisha Taasisi ya Uhasibu (TIA) na
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Robo fainali ya mwisho itakayoanza saa 9 kamili itakuwa kati ya
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Utumishi Magogoni.
Washindi watacheza nusu fainali Jumapili (Mei 11 mwaka huu) kwenye ufukwe huo
huo.
Mechi za kutafuta mshindi wa tatu, na ile ya fainali zitachezwa
kwenye ufukwe huo huo wikiendi ya Mei 17 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment