Klabu ya Young Africans
imeeingia makubaliano na Benki ya Posta nchini juu ya mabadiliko ya
utengenezaji wa kadi za wanachama kutoka kwenye mfumo wa zamani
(analogy) kwenda kwenye mfumo mpya wa kisasa (digital) ambapo sasa
wanachama wake watakua wakitumia kadi zenye mfumo wa ATM.
Mkurugenzi Masoko wa Benki ya
Posta nchini Bw. Deo Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada
ya kukaa na viongozi na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza
mapatao kwani wigo wake wa kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa
nchi nzima na kwa muda mfupi.
“Badala ya wanachama kuja Dar
es salaam makao makuu kujaza fomu za uanachama watakua wanaweza kufanya
hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi za Benki ya Posta na kujaza fomu
hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama” alisema Deo.
Gharama za kujiunga na uanchama
zitabakia zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya mwaka elfu Tshs 12,000/=
ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB yenye logo ya timu yake
ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI kwa huduma ya kuweka na
kutoa fedha.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Klabu
ya Yanga Clement Sanga amesema anaishukuru Benki ya Posta kwa kuweza
kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo huu wa kisasa tutaweza
kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi zaidi na taarifa zetu
zitaweza kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.
Uzinduzi rasmi wa kadi mpaya za
uanachama utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye hoteli ya Hyatt Kempsinki
eneo la Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na mara baada ya uzinduzi moja
kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama kutoka kwenye mfumo wa analogy
kwenda digital utaanza.
CHANZO: TOVUTI YA YANGA
No comments:
Post a Comment