STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 6, 2014

Yanga kuwavaa Wamalawi, Simba kupimana na Gor Mahia leo


Yanga
http://3.bp.blogspot.com/-OfEoDMBLCgk/UsRjBepOVNI/AAAAAAAA9DU/4oSvu7sBJ8Q/s1600/IMG_7008.JPG
Simba
WAKATI watani zao wa jadi wakishuka dimbani leo kuvaana na Gor Mahia ya Kenya, timu ya Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani kesho kuwavaa Wamalawi wa timu ya Big Bullets (zamani Bata Bullets).
Mechi zote mbili zitachezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zikiwa ni za kirafiki za kimataifa kujiandaa na Ligi Kuu itakayoanza wiki mbili zijazo.
 Yanga itashuka dimbani kesho ikiwa ni siku chache baada ya kutoka kuwagonga, Thika United bao 1-0 katika mechi nyingine ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa  Taifa.
Mechi hiyo itachezwa kuanzai saa 10 jioni na viingilio vyake vitakuwa kama ifuatavyo:
VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/=
Orange Tshs 10,000/=
Blue & Green Tshs 5,000/=
Wakati huo huo Simba itashuka dimbani leo kuvaana na Gor Mahia katika mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Taifa, na Wakenya hao tayari wameshatua Bongo tangu jana tayari kwa mechi hiyo.
Hiyo itakuwa mechi ya kwanza ya kocha Patrick Phiri kwenye uwanja wa Taifa akitoka kumrithi Zdravkov Logarusic aliyetimuliwa siku moja baada ya kipigo cha mabao 3-0 toka kwa ZESCO siku ya Simba Day.
Simba waliokuwa wameweka kambi ya mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu visiwani Zanzibar imeshatua jijini Dar es Salaam tayari kuwavaa Wakenya hao na kuwaonyesha mashabiki wao baadhi ya vifaa vipya vilivyosajiliwa wakti timu ikiwa kambini.

No comments:

Post a Comment