STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 6, 2014

Simanzi! Ajali yachinja 39, wengine 75 hoi


AJALI ya kutisha iliyohusisha magari matatu yakiwamo mabasi mawili ya abiria na gari ndogo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 39 huku wengine zaidi ya 70 wakiwa majeruhi.
Mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yaligongana uso kwa uso na kuumia vijana katika eneo la Sabasaba, Musoma mjini na kusababisha simanzi katika eneo la tukio kutokana na miili ya abiria na madereva pamoja na makondakta wa magari hayo kukatikakatika vibaya.
Mabasi hayo moja lenye nambaza usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Sirari, Mara na Mwanza Coach lenye nambari za usajili T 736 AWJ yaligongana uso kwa uso. Kwa mujibu taarifa toka eneo la tukio na kuthibitisha na Polisi Mkoa wa Mara, zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo, kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.
Hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.
Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu, ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 39 kupoteza maisha pamoja hapo wakishuhudia tukio hilo la ajali.

Buldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni. Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.
Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.

No comments:

Post a Comment