
Muller alifunga bao la kwanza katika dakika ya 18 ya mchezo, kabla ya Ikechi Anya akaisawazishia Scotland katika dakika ya 66.
Baada ya matokeo kuwa 1-1, Ujerumani ambao ni mabingwa wa kombe la dunia chini ya kocha Joachim Low walifanya mashambulizi kadhaa langoni kwa Wascotish na katika dakika ya 70, Muller aliandika bao la pili na la ushindi.
Mabao hayo yamemfanya Muller kufikisha jumla ya 25 katika mechi 58 alizoichezea timu ya Taifa ya Ujerumani.
Katika mchezo huo Scotland walipata pigo katika dakika za majeruhi baada ya Charlie Mulgrew kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
No comments:
Post a Comment