STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 28, 2014

Mtibwa Sugar yaendeleza rekodi Ligi ya Bara

* Ruvu Shooting yaizamisha JKT Ruvu

* Yanga, Azam zashikana mashati Taifa

* Mpaka sasa mabao 2-2

Mtibwa Sugar
http://3.bp.blogspot.com/-c8YFHqfoGQ0/UXZpy7CgJtI/AAAAAAAAHIk/Nf9mAwQFKoM/s640/DSC_0125.JPG
JKT Ruvu waliochezea kichapo usiku wa jana kwa Ruvu Shooting
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mtibwa Sugar imeendeleza rekodi yake ya kuwa imu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote msimu huu, baada ya asubuhi ya leo kulazimisha sare ya bao 1-1 na Stand United baada ya mchezo huo kushindwa kuendelea kuchezwa jana sababu ya mvua kubwa.
Pambano hilo lilichezwa jana kwa dakika sita na kurudiwa leo asubuhi dakika zilizosalia kwa timu hizo kushindwa kutambiana kwenye uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro.
Wageni Stand ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Shaaban Kondo aliyefunga katika dakika ya 22, kabla ya Mtibwa kusawazisha katika dakika ya lala salama kupitia beki wake Saidi Mkopi na kuifanya timu hiyo iendelee kukaa kileleni ikiwa na pointi 16 baada ya mechi nane, ingawa inaweza lkujikuta iking'oka kileleni kama Yanga inayoumana na Azam itapata ushindi katika mchezo wao.
Azam pia ina nafasi ya kukwea kileleni kama itaishinda Yanga kwa uwiano mzuri wa mabao, ingawa hadi sasa timu hizo zimefungana mabao 2-0.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Didier Kavumbagu kabla ya Amissi Tambwe kusawazisha kwa kichwa dakika chjache baadaye na katika kipindi cha pili, Simon Msuva aliiongezea Yanga bao la pili dakika ya 53 kabla ya John Bocco kufunga bao la kusawazisha hivi punde.
Katika mechi nyingine ya jana ya ligi hiyo Ruvu Shooting iliendelea ubabe wake kwa JKT Ruvu baada ya kuichapa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa usiku kwenye uwanja wa Chamazi.
Bao pekee la Ruvu liliwekwa kimiani kwa mkwaju wa penati na Hamis Kasanga na kuifanya timu hiyo kufiksiha pointi 10 na kulingana na 'ndugu zap hao wa JKT ila wanatofautiana kwa mabao ya kufunga nba kufungwa.

No comments:

Post a Comment