STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 28, 2014

Salha wa Hammer bado aota albamu na mumewe

Salha Abdallah
Salha Abdallah na mumewe, Hammer Q
MUIMBAJI mahiri wa taarab nchini  Salha Abdallah 'Salha wa Hammer' amesema licha ya kurejea kwenye muziki wa makundi, bado ataendelea kushirikiana na mumewe kutengeneza kazi zao binafsi.
Salha aliyejiunga na kundi la Five Star akitokea kwenye likizo ya uzazi alisema kuwa, bado mipango ya kutengeneza albamu ya pamoja na mumewe ipo pale pale japo anaendelea kupiga mzigo kazini kwake.
Muimbaji huyo wa zamani wa Dar Modern na aliyekuwa akilifanyia kazi King' s Modern kabla ya kwenda likizo ya uzazi, alisema kurejea kwake kwenye makundi hakuna maana kumemzuia mipango yake.
"Sidhani kama kurejea kwangu kuiimbia makundi kutanizuia kuendelea na mipango yangu na mwenza wangu kutengeneza albamu, nitaendelea nayo," alisema.
Wanandoa wao walishaachia nyimbo za 'Tunapendana' na 'Safiri Salama' na walikuwa katika mipangop ya kukamilisha nyimbo nyingine kuhitimisha albamu yao kabla ya Salha kupata likizo ya uzazi.

No comments:

Post a Comment