STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 28, 2014

Yanga, Azam zashindwa kuing'oa Mtibwa kileleni

* Polisi Moroyainyoa Mgambo 2-0

* Mbeya City yainyuka Ndanda yatoka mkiani

http://1.bp.blogspot.com/-s5DKJ66I-uI/VKASWSksnnI/AAAAAAAG6Ik/eJj5rbWvwok/s1600/MMGM0086.jpg
Tambwe akifunga bao la kusawazisha la Yanga
http://1.bp.blogspot.com/-zjoebZty438/VKARRDjm0iI/AAAAAAAG6IM/E6B43jVIZA8/s1600/MMGM0090.jpg
Tambwe akishangilia bao lake sambamba na Simon Msuva ambaye pia aliifungia Yanga bao la pili
Azam wakishangilia bao lao la kwanza dhidi ya Yanga leo kwenye uwanja wa Taifa
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/08/Mbeya-City.jpgPAMBANO la kukata na shoka baina ya Yanga na Azam limemalizika matokeo yakiwa ni yale yale ya mabao 2-2 na kuendelea kuwa nyuma ya Mtibwa Sugar wanaoongoza msimamo.
Yanga walikuwa 'nyumbani' walitanguliwa kufungwa bao dakika ya tano na Didier Kavumbagu baada ya mabeki wa Yanga kuchanganyana na kipa wao Deo Munishi 'Dida' na kumpa nafasi nyota huyo wa zamani wa Jangwani kukwamisha bao kirahisi.
Yanga walicharuka dakika mbili baadaye Amissi Tambwe aliisawazishia Yanga bao baada ya kuunganisha mpira wa krosi iliyopigwa na kiungo Salum Telela na kufanya matokeo yadumu hivyo hadi mapumziko.
Yanga iliingia kipindi cha pili wakiwa wamecharuka na kuandika bao la pili dakika ya 52 kupitia Simon Msuva aliyeunganisha kwa kichwa bao lililotokana na pasi murua ya Haruna Niyonzima aliyeshirikiana vema awali na Kpah Sean Sherman aliyeonekana tishio langoni  mwa Azam muda wote wa mchezo huo.
Hata hivyo nahodha John Bocco aliyekuwa akitokea benchi mpira wake wa kwanza kuugusa uwanjani ulizaa bao la kusawazisha la Azam baada ya mabeki wa Yanga kujichanganya tena na mchezaji huyo aliyekuwa majeruhi kufunga kirahisi kwa kichwa mpira wa krosi ya Himid Mao dakika ya 65.
Kwa matokeo hayo Yanga imeendelea kung'ang'ania nafasi ya pili nyuma ya Mtibwa ikiwa na pointi 14 sawa na zile za Azam isipokuwa wanatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Matokeo ya mechi nyingine Polisi Moro imeifyatua Mgambo JKT ya Tanga kwa mabao 2-0, mabao katika pambano hilo yalifungwa na Nicolaus Kibopile katika dakika ya 21 na Imani Mapunfda aliyekwamisha bao la ushindi dakika ya 85, huku Mbeya City ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara na hivyo kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment