STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 28, 2014

Chelsea chupuchupu, yalazimisha sare ugenini

Sadio Mane  akishangilia bao la Southampton
Eden Hazard akishangilia bao la kusawazisha la Chelsea
VINARA wa Ligi Kuu ya England, Chelsea imeponea chupuchupu leo ugenini baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton katika pambano lililomalizika muda mfupi uliopita.
Southampton waliwakaribisha Chelsea katika uwanja wa St Mary kwa bao la mapema la dakika ya 17 kupitia kwa Sadio Mane kabla ya Chelsea kuchomoa dakika chache kabla ya mapumziko kupitia kwa Eden Hazard akimalizia kazi nzuri ya Cesc Fabregas.
Southampton ilijikuta ikicheza pungufu baada ya Morgan Schneiderlin kuonyesha kadi nyekundu dakika chache kabla ya kumalizika kwa pambano hilo

Kwa sare hiyo Chelsea wameendelea kung'ang'ania kileleni wakiwa na pointi 46, baada ya mechi 19 na kwa sasa mechi nyingine zinaendelea ambapo Manchester City wanaoongoza mabao 2-1 dhidi ya Burnley huku Arsenal ikiwa ugenini inaoongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United.

No comments:

Post a Comment