STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 7, 2014

TFF yaziombea baraka Yanga, Azam kufanya kweli Afrika

Yanga
Azam Fc
 SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazitakia kila la kheri klabu za Yanga na Azam ambazo timu zake zinatuwakilisha kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).

Yanga inacheza na Komorozine ya Comoro katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya CL itakayochezwa kesho (Februari 8 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Nayo Azam inaikaribisha Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya CC utakaochezwa Jumapili (Februari 9 mwaka huu) saa 10 kamili kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Ni matumaini yetu kuwa timu hizo mbili zitatuwakilisha vizuri kwenye michuano hiyo, na kuwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi viwanjani kuziunga mkono hasa kwa vile zinacheza nyumbani.


Wapinzani wa timu hizo tayari wameshawasili tayari kwa mechi hizo ambazo wawakilishi hao wa Tanzania wanahitaji kupata ushindo mnono ili kuwa na kazi nyepesi mechi zao za marudiano. 

No comments:

Post a Comment