STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 7, 2014

Prisons, Ruvu hapatoshi Mbeya kesho, FDL kutimka

Kikosi cha Prisons-Mbeya


Ruvu Shooting

Na Boniface Wambura
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 8 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi nyingine nne za ligi hiyo zitachezwa keshokutwa (Februari 9 mwaka huu) kwenye viwanja mbalimbali.
Mgambo Shooting vs Simba (Mkwakwani, Tanga), Oljoro JKT vs Kagera Sugar (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Rhino Rangers vs Coastal Union (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na Mbeya City vs Mtibwa Sugar (Sokoine, Mbeya).
Katika hatua nyingine, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) unaanza kesho (Februari 8 mwaka huu) kwa mechi za kundi A na B wakati kundi C lenyewe litaanza mechi zake Februari 22 mwaka huu. Mechi za kundi A ni Green Warriors vs Tessema (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi), Polisi Dar es Salaam vs Transit Camp (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam). Februari 9 mwaka huu ni African Lyon vs Villa Squad (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi) na Friends Rangers vs Ndanda (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam). Kundi B kwa kesho (Februari 8 mwaka huu) ni Polisi Morogoro vs Burkina Faso (Jamhuri, Morogoro), Lipuli vs Mkamba Rangers (Samora, Iringa), Kurugenzi vs Kimondo (Wambi, Mufindi) na Mlale JKT vs Majimaji (Majimaji, Songea).

No comments:

Post a Comment