Kocha Kibadeni akiwaonyesha wachezaji wake kipi cha kufanya katika mazoezi ya leo asubuhi |
Kocha msaidizi, Amri Said, akionyesha cha kufanya kwa wachezaji wake |
King Kibadeni achaneni naye yupo 'serious' mazoezini si mchezo |
Beki mpya wa Simba, Issa Rashid 'baba Ubaya' akijifua na wenzake |
Wachezaji wa Simba wakijifua huku kocha wao, Amri Said (6) akiwaangalia |
Hussein Ibrahim Twaha 'Messi' yuko kikazi zaidi licha ya kusumbuliwa na kifua |
mchezaji anayedaiwa kutoka Zimbabwe, Tinash akijifua na wenzake leo asubuhi |
KLABU ya soka ya Simba inaendelea kujifua kwenye uwanja wa Kinesi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika nchini Sudan, huku idadi ya wachezaji wanaojitokeza kuomba kupata nafasi ya kusajiliwa ikizidi kuongezeka wakiwamo wageni, ambapo Wanigeria na Mzimbabwe ni kati yao.
Wanigeria wanaojifua katika mazoezi hayo yanayosimamiwa na jopo la makocha watano wakiongozwa na King Abdallah Kibadeni akisaidiwa na Jamhuri Kihwelu 'Julio' Njames Kisaka, Amri Said na Seleman Matola ni pamoja na Modebe Izze na Samuel Okey wakati Mzimbabwe ni Tinash Motenence.
Wachezaji hao wanashindana na Wakongo wanne waliojitokeza tangu siku ya kwanza ya utambulisho wa Kibadeni kwa wachezaji hao na wanaendelea kupimwa na makocha hao kwa ajili ya mmoja wao kusajiliwa kuziba nafasi ya mchezaji mmoja wa kigeni iliyosalia Msimbazi.
Kocha msaidizi wa Simba, Julio alisema kwa sasa wamesaliwa na nafasi moja tu ya mchezaji wa kigeni na hivyo wataangalia mwenye uwezo wa kubebeshwa nafasi hiyo akisema wanamhitaji zaidi kiungo.
Julio alisema mpaka sasa bado hawana la kusema kuhusu wachezaji hao kwa vile ndiyo kwanza wanaanza kuwapima, lakini alisema miongoni mwa waliojitokeza wapo wenye uwezo mkubwa na kuwapa matumaini ya kupata kikosi imara kitakachoungana na wale walioichezea timu hiyo msimu huu ili kuweza kushiriki vyema Kagame na ligi ya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment