Haruna Shamte wakipashaa misuli na mchezaji mwenzake |
King Kibadeni akiwa makini kwenye mazoezi ya Simba |
Mwaka huu watatukoma: Baadhi ya viongozi wa Simba wakifuatilia mazoezi ya timu yao. (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu, Evodius Mtawala |
Baba Ubaya akionyesha 'ubaya' wake mazoezini |
Vikosi vyetu vya kupima ubavu vitakuwa hivi: Makocha wasaidizi wa Simba, Julio na Kisaka wakijadiliana leo asubuhi wakati wa mazoezi ya timu yao |
Samuel Ngassa naye yumo mazoezni Simba |
Messi aliyeipa kamera mgongo na mwenzake |
Yule mrefu anatufaa: Julio na Kisaka pamoja na Amri said (6) makocha wasaidizi wa Simba wakiwa kazini |
Rukeni hivi:Kibadeni akiwaelekeza kwa mfano wachezaji wake |
Mtanikoma! Messi kutoka Coastal akionyesha balaa mazoezini |
Lazima mtunyakue tu mtake msitake |
Kila mmoja anaonyesha makeke yake, huyu ni Haruna Shamte |
Messi akiongoza wenzake |
Shamte na mwenzake wakifanya mazoezi ya viungo |
BAADHI ya wanachama wa klabu ya Simba wameifagilia Kamati ya Usajili ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Zakaria Hanspope kwa kufanya usajili mzuro waliodai unawapa matumaini ya kufanye vyema kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao na hata kwenye michuano ya Kagame.
Pia kamati hiyo imefagiliwa zaidi kwa kuepuka kusajili wachezaji wanaotoka kwa mahasimu wao Yanga, kwa kudai watasaidia kujenga timu yenye nidhamu na mipango itakayoweza kurejesha heshima ya klabu yao.
Mmoja wa wanachama hao, Onesmo Waziri 'Ticotico' aliyewahi kuwa Katibu wa Kamati ya Fedha na Mipango chini ya uongozi wa sasa, alisema amefurahishwa mno na namna usajili wa Simba unavyofanyika.
Waziri alisema ni vyema kamati yao ya usajili ikaendelea na mwenendo huo huo wa kusajili kwa umakini mkubwa na kuepuka kuchukua mchezaji yeyote kutoka Yanga ili waijenge timu katika nidhamu moja itakayoinufaisha timu yao kwa michuano itakayoshiriki.
"Nafurahi sana kuona Simba wanafanya usajili wenye akili kuliko ule uchafu tulioufanya msimu uliopita, lakini niwapongeze zaidi kamati kwa kuachana na tabia ya kusajili wachezaji kutoka Yanga," alisema.
Aliongeza;."Unasajili wachezaji wenye upeo mdogo kama (jina kapuni) maana yake ni kutafuta matatizo napenda wasonge mbele tupate wachezaji wengine wenye viwango vipya na mawazo mapya. Simba tunaweza sana tena sana."
Mwanachama mwingine aliyejitambulisha kama Bakar Ally wa Tawi la Ubungo, alisema kwa mwenendo wanaoenda nao uongozi wao kwa kusajili kwa umakini wanawapa matumaini ya kurejesha heshima yao hasa ikizingatiwa timu ipo chini ya King Abdallah Kibadeni mmoja wa makocha wenye mafanikio nchini.
Pongezi hizo za wanachama hao wa Simba zimekuja wakati kamati hiyo ikitangaza baadhi ya wachezaji iliyowanyakua mpaka sasa ikiwamo Mganda Mosse Oloya, Ibrahim Twaha 'Messi', Issa Rashid 'Baba Ubaya' na kipa kutoka Kagera Sugar.
No comments:
Post a Comment